Barabara katika mpaka wa Tunduma Kutanuliwa Waziri lega atoa maagizo

 Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega ameagiza Wakala wa Barabara (TANROADS), kufanya tathmini ya kutanua barabara katika mpaka wa Tunduma unaopitisha magari yaendayo nchi jirani za Zambia na DR Congo ili kupunguza msongamano wa magari katika eneo hilo.


Ulega ametoa agizo hilo akiwa Tunduma mkoani Songwe na kueleza kuwa Serikali inatambua changamoto wanayopitia wasafirishaji na wananchi wa eneo hilo kutokana na msongamano wa malori kwa muda mrefu na kukwamisha matumizi ya barabara kwa watumiaji wengine.

Kuhusu changamoto ya Mzani wa Mpemba unaosababisha magari kugeuza ili kupima uzito, Waziri Ulega amesema Wizara ya Ujenzi inakwenda kujenga mzani mwingine katika eneo la Iboya ili kuruhusu magari yote yanayotoka Tunduma kwenda Mbeya kupima uzito katika mzani huo na hivyo utapunguza msongamano wa malori.

Aidha, Ulega amewataka mameneja wa TANROAS wa mikoa ya Mbeya na Songwe kuhakikisha wanaimarisha barabara za mchepuo ambazo kwa kiasi kikubwa zitapunguza foleni ya magari katika ukanda huo.


Post a Comment

Previous Post Next Post