Na Bakari Lulela
WANAWAKE zaidi ya 200 wanaojihusisha na utengenezaji wa bidhaa za batiki wamenufaika na Mafunzo ya usalama na Afya yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kufanya shughuli zao za kila siku kwa kuzingatia kanuni bora za Usalama na Afya Mahali pakazi.
Mafunzo hayo ya siku moja yaliyogharamiwa na Serikali yametolewa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pakazi (OSHA) katika eneo la Ilala jijini Dar es salaam ambapo mada mbalimbali zikiwemo Dhana ya Usalama na Afya Mahali pakazi, vihatarishi vya Usalama na Afya katika shughuli za uzalishaji bidhaa za batiki pamoja na huduma ya kwanza Mahali pakazi zimefundishwa.
Mafunzo hayo yamefunguliwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu_kazi,Ajira na Mahusiano Rahma Kisuo ambaye ameelezaea umuhimu wa Mafunzo ya usalama na Afya Mahali pakazi kwa makundi ya Wajasiriamali wadogo huku akiitaka OSHA kuhakikisha Mafunzo hayo yanakuwa endelevu .
"Wajasiriamali wadogo ni kundi muhimu sana na lenye mchango mkubwa katika kukiza uchumi wa Taifa letu hivyo ni muhimu kuwapatia Mafunzo Ili waweze kutekeleza shughuli zao katika hali ya usalama," amesema Naibu Waziri.
Aidha, amesisitiza kuwa Mafunzo hayo yatasaidia kupunguza ajali, Magonjwa na video vinavyoweza kutokea kutokana na ukosefu wa mifumo ya usalama na Afya ikiwemo wafanyakazi wenye uelewa wa masuala husika.
Sambamba na hayo, ametoa wito kwa wafanyabiashara hao kutojihusisha na makundi yenye Nia ya kuvuruga shughuli za uzalishaji na kuvunja amani ya nchi ya Tanzania.
Awali, Mtendaji Mkuu wa OSHA Khadija Mwenda, amesema Mafunzo hayo ni mwendelezo wa utekelezaji wa program ya afya Yangu_ Mtaji wangu ili kuziba mwanya wa uelewa wa masuala ya Usalama na Afya uliopo baina ya sekta rasmi na sekta isiyo rasmi hivyo kupitia program hii tumekuwa tukiainisha makundi mbalimbali ya Wajasiriamali wadogo na kuwawezesha kwa Mafunzo pamoja na kuwapatia vifaa kinga muhimu kutegemeana na aina ya shughuli zao.," amesema Mtendaji Mkuu wa OSHA.
Aidha, amesema program hiyo itaendelea kutolewa kwa makundi mbalimbali hususani vijana ambao kwa mujibu wa tafiti za OSHA za hivi karibuni ndio waathirika wakubwa wa ajali katika maeneo ya uzalishaji kutokana na uelewa mdogo na ukosefu wa uzoefu kazini.
Akitoa maoni yake katika Mafunzo hayo mmoja wa washiriki wa Mafunzo hayo ,Jesca Charles ameishukuru OSHA kwa kuwapatia elimu na vifaa kinga ambavyo vitawasaidia kujikinga dhidi ya vihatarishi vya ajali na Magonjwa hususani kemikali ambacho ndio kihatarishi kikubwa katika uzalishaji wa bidhaa za batiki.
Tags
KITAIFA