BAKWATA YASAMBAZA ZANA ZA UCHAGUZI MKUU 2026, VIONGOZI WATAKIWA KUWA MAKINI


Na Omari Janja

DAR ES SALAAM - Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) tayari limeanza kusambaza vifaa na zana za awamu ya pili kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa viongozi wa baraza hilo unaotarajiwa kufanyika mwaka huu wa 2026, huku viongozi wa ngazi mbalimbali wakitakiwa kufuata taratibu uliowekwa li kufanikisha uchaguzi huo.

Akizungumza na Wandishi wa Habari, Afisa Utawala wa BAKWATA Makao Makuu ambaye pia ni kiongozi mwandamizi wa uchaguzi huo, Mwalimu Rashid Kassim Mohamed, amesema maandalizi ya kutosha yameshafanyika, ikiwemo kukamilika kwa semina za awali zilizohusisha viongozi wa kitaifa, mikoa, na wilaya. Bofya hapa Kuazama Video Kamili.

Amesema kuwa, baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza iliyohusisha usambazaji wa fomu za kuomba uongozi, hivi sasa baraza limetoa zana za awamu ya pili ambazo ni pamoja na karatasi za kupigia kura (ballot papers), vyeti vya ushindi (winning certificates), pamoja na fomu za malalamiko (claim forms) kwa ajili ya ngazi mbalimbali.

Mwalimu Rashid amesema uchaguzi huo umegawanyika katika maeneo makuu matatu ambayo ni upande wa BAKWATA, unaojumuisha ngazi za mikoa, wilaya, kata, na misikiti), pamoja na Jumuiya mbili ambazo ni Jumuia ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania (JUWAKITA) na Jumuia ya Vijana (JUVIKIBA), ambapo fomu zao maalum za kamati na vyeti vya ushindi vimeshasambazwa mikoani hadi ngazi za chini.

Kuhusu fomu za malalamiko (claim forms), kiongozi huyo alieleza kuwa zimetolewa mahususi kwa ajili ya watu ambao hawatarihika na hatua yoyote ya uchaguzi, ambapo watatakiwa kuzijaza na kuzikabidhi katika ofisi husika ndani ya muda uliopangwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi huo.

Katika hatua nyengine Mwalimu Rashid amewasisitiza viongozi wote walioko mikoani, wilaya, kata, hadi ngazi ya msikiti kuhakikisha kila hatua inafanywa kwa umakini mkubwa, na kuwasihi wasisite kuwasiliana na makao makuu au kumpigia Katibu Mkuu moja kwa moja endapo watakuwa na uhitaji wa maelezo ya ziada au ufafanuzi.


Post a Comment

Previous Post Next Post