Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limemchagua Rais wa Klabu ya Yanga SC na Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu Afrika (ACA), Eng. Hersi Said, kuwa miongoni mwa wataalamu watakaowasilisha mada kwenye kongamano kubwa la mpira litakalofanyika Doha, Qatar, kesho, Desemba 14, 2025.
Eng. Hersi amepangiwa kutoa mada uhusuyo “Key Elements for Club Successful Transformation (Njia Muhimu za kufanya Mabadiliko yenye Mafanikio katika Klabu)”, huku akichangia uzoefu wake wa kimataifa.Miongoni mwa wataalamu wengine wa mpira watakaozungumza kwenye kongamano hilo ni Arsene Wenger, Roberto Di Matteo, Dennis Wise, Alexander Pato, Eric Abidal, pamoja na wengine kadhaa. Eng. Hersi Said ndiye mtaalamu pekee kutoka Afrika aliyepata nafasi ya kumwaga 'madini' kwenye kongamano hilo kesho.
.jpg)